SiasaAsia
Ushuru wa Marekani utaziathiri zaidi nchi zinazoendelea
12 Aprili 2025Matangazo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Biashara ya China, Wentao amesema Marekani imeendelea kuchukua hatua za kuongeza ushuru na kusababisha hali ya sintofahamu na ukosefu wa utulivu wa masoko ya biashara duniani hatua inayoleta mtafaruku kimataifa na hata ndani ya Marekani.
Soma zaidi: China yaomba mshikamano na EU kuukabili ushuru wa Donald Trump
Ameyasema hayo siku chache baada ya China kutangaza ushuru wa asilimia 125 kwa bidhaa za Marekani zinazoingizwa nchini mwake unaoanza kutumika Jumamosi 12.04.2025. Awali, Marekani iltangaza kuwa imepandisha ushuru wake kwa bidhaa za China kwa asilimia 125.