China, Urusi na Iran wairai Marekani kuiondolea vikwazo Iran
14 Machi 2025
Badala yake, mataifa hayo yametaka mazungumzo yafanyike kuhusu suala hilo. Katika taarifa ya pamoja ilisomwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Ma Zhaoxu, akiwa na manaibu waziri wenzake wa Urusi, Ryabkov Sergey Alexeevich na wa Iran Kazem Gharibabadi, imesema mataifa hayo matatu yaliyokutana leo mjini Beijing yalisisitiza umuhimu wa kusitisha vikwazo vyote visivyo halali vya upande mmoja.
''Tumesisitiza kuwa mazungumzo ya kisiasa na kidiplomasia yanayozingatia kanuni za kuheshimiana kwa wote yanabaki kuwa chaguo la pekee linaloweza kuaminika na kutekelezwa kuhusiana na suala hilo.'' amesema Ma.
Mazungumzo hayo ni jaribio la hivi karibuni zaidi la kuangazia suala hilo na yanafanyika baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kumwandikia barua kiongozi wa ngazi ya juu wa Iran kwa lengo la kuanza tena mazungumzo.