China na Marekani kujadili mvutano wa kibiashara
10 Juni 2025Matangazo
Maafisa wa Marekani na China wanajiandaa kukutana kwa siku ya pili leo Jumanne kwa mazungumzo ya kibiashara mjini London, nchini Uingereza.
Mazungumzo hayo yanalenga kutafuta makubaliano kuhusu suala tete la ushuru chini ya kiwingu cha mvutano uliozidishwa na ongezeko la masharti ya usafirishaji bidhaa.
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng anaongoza ujumbe wa nchi hiyo akiandamana na Waziri wa Biashara Wang Wentao wakati ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Waziri wa Fedha Scott Bessent, na Waziri wa Biashara Howard Lutnick.
Mkutano huo wa London unafanyika baada ya Marekani kuishutumu China kwa kukiuka makubaliano yao yaliyofikiwa Geneva, Uswisi, ya kumaliza mvutano kuhusu ushuru.