China na Kenya zatangaza kuimarisha zaidi mahusiano
24 Aprili 2025Rais Xi amesema uamuzi wa kuyaboresha zaidi mahusiano ya Kenya na China umefanyika wakati ambapo kuna msukosuko wa kimataifa.
Kenya imekuwa nchi inayopata manufaa makubwa kutokana na mpango wa China wa Ujenzi wa barabara uliozinduliwa mwaka 2013 ili kutanua ushawishi wa kikanda na kiuchumi wa China kupitia ujenzi wa miundo msingi duniani.
"Ni furaha yangu kuendelea kujenga kutokana na kile kilichoko tayari, kuleta maelewano mazuri kati ya watu wetu na kuhakikisha kwamba tunayapeleka haya katika siku zijazo. Katika safari hiyo kwa pamoja tumefanikiwa katika mengi," alisema Ruto.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Xi na Ruto wamesaini nyaraka 20 kwa pamoja Alhamis. Nyaraka hizo zimejumuisha makubaliano ya ushirikiano wa sayansi na teknolojia, sekta ya reli na biashara ya mtandaoni.