China, Korea Kusini na Japan zaimarisha biashara huria
30 Machi 2025Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano wa maafisa wao wakuu wa kibiashara ambao ni wa kwanza kufanyika ndani ya miaka mitano, ikiwa ni siku kadhaa kabla ya kuanza utekelezwaji wa ushuru mpya kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani ikiwemo magari, malori na sehemu za magari.
Trump atangaza ushuru mpya wa magari yanayoagizwa kutoka nje
Mkutano huo uliohudhuriwa na waziri wa viwanda wa Korea Kusini Ahn Duk-geun, mwenzake wa Japan na china Yoji Muto na Wang Wentao, ulikubaliana kuanzisha ushirikiano huo wa kibiashara haraka pamoja na uwekezaji. Waziri Ahn amesema nchi hizo tatu ni lazima ziitikie kwa pamoja wito wa kutatua changamoto zao za pamoja.
Korea Kusini na Japan ni wauzaji wakubwa wa magari huku China nayo ikiathiriwa pia na ongezeko hilo la ushuru kutoka Marekani.