China, Iran, Urusi zajadili ushirikiano sekta ya ulinzi
26 Juni 2025Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa China, Dong Jun ameyataja mazungumzo hayo kuwa ni ya kukabiliana na dunia iliyo katika mparaganyiko na iliyokosa utulivu. Amewataka washirika wake kushirikiana na kuchukua hatua madhubuti zaidi ili kulinda mazingira yatakayoleta amani.
Soma zaidi: Iran, China na Urusi kuanza luteka za pamoja za kijeshi
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belousov aliyekutana na Dong kando mwa mkutano rasmi amepongeza ushirikiano kati ya China na Urusi na kusema ushirikiano wa nchi zao uko katika kiwango cha juu. Yanaendelea pia ikiwa ni siku moja baada ya viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kumaliza mkutano wao huko Uholanzi ambapo nchi wanachama zimekubaliana kuongeza bajeti ya ulinzi.