BiasharaAsia
China yatathmini kufanya mazungumzo ya ushuru na Marekani
2 Mei 2025Matangazo
Hata hivyo imesisitiza kuwa ni lazima Marekani iwe tayari kuufuta ushuru ambao umeyatikisa masoko na njia za usambazaji wa bidhaa kabla ya kuanza mazungumzo.
Soma zaidi: China yasema haiogopi vita ya kibiashara na Marekani
Marekani imeiadhibu China kwa kupandisha ushuru wa bidhaa zake nyingi zinazoingizwa nchini humo kwa asilimia 145 tangu mwezi Aprili wakati China imejibu hatua hiyo kwa kuziwekea ushuru wa asilimia 125 bidhaa zinazotoka Marekani.
Soma zaidi: China: Ushuru wa Marekani utasababisha madhara makubwa kwa nchi zinazoendelea
Rais wa Marekani Donald Trump mara kadhaa amedai kuwa China imekuwa ikiomba kufanya maazungumzo kuhusu ushuru huo na wiki hii alisema kuwa kuna uwezekano mzuri kuwa nchi hizo mbili zitapata makubaliano.