China: BRICS haitaki malumbano na Rais Donald Trump
7 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning, amesema nchi yake inasisitiza msimamo wake kwamba hakuna mshindi katika vita vya kibiashara na kuongezeana ushuru.
Hata hivyo Trump amesema atapeleka barua za kwanza hii leo Jumatatu (07.07.2025), kwa nchi kadhaa kuhusu swala la ongezeko la ushuru huku zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika muda alioutoa wa kufikia makubaliano na washirika wa kibiashara.
Mkutano wa BRICS mjini Rio waukosoa ushuru wa Trump
Licha ya BRICS, inayojumuisha Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, kugawanyika kuhusu masuala mengi, imeungana katika msimamo dhidi ya utawala wa Rais wa Marekani na vita vyake vya ushuru vinavyokatizwa na kuanzishwa kila mara.