China yakosoa mpango wa Marekani kwa wanafunzi wake
29 Mei 2025Matangazo
Awali Marekani ilisema itaondoa nafasi ya wanafunzi hao kuomba visa za kuingia nchini mwake. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning, amesema tayari wamewasilisha malalamishi yao kwa utawala wa Trump.
Visa za wanafunzi hao zinachangia kiwango kikubwa cha mapato ya vyuo vikuu nchini Marekani.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio amesema taifa lake pia litaimarisha ukaguzi wa visa wa wanafunzi wote kutoka China na Hong Kong
Marekani imechukua uamuzi huo kutokana na maandamano ya mara kwa mara ya wanafunzi katika vyuo vikuu.