JamiiChile
Chile: Juhudi zapamba moto kuwaokoa wachimba madini
2 Agosti 2025Matangazo
Maporomoko hayo yalitokana na eneo moja la mgodi huo kukumbwa na tetemeko la ardhi.
Zaidi ya waokoaji 100 wanashiriki katika harakati hizo kabambe na kwa mujibu wa taarifa ya shirika la serikali la uzalishaji wa shaba nchini Chile, waokoaji hao wameshafika mita 4 kuelekea kwa wachimba madini walionaswa chini ya mgodi.
Hata hivyo shirika hilo ”Coledo” limesema bado haijawezekana kuwasiliana na wachimba migodi hao walionaswa mita 53 chini ya mgodi. Shughuli katika mgodi huo zimesitishwa kufuatia ajali hiyo.