Chelsea yashinda Kombe la Dunia la Vilabu
14 Julai 2025Matangazo
Ushindi huo wa Chelsea kwenye dimba la MetLife mjini New Jersey umewaacha wengi vinywa wazi. Licha ya kutinga fainali, kulikuwa na matumaini madogo miongoni mwa wachambuzi wa soka duniani kuwa Chelsea ingemudu kulitwaa kombe hilo mbele ya PSG, ambayo mwezi Mei walinyakua kombe la michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, Champions League.
Hata hivyo magoli mawili ya Cole Palmer na jingine la Joao Pedro yaliyotiwa wavuni mnamo dakika 45 za kwanza yalisadifu kuwa kihunzi ambacho PSG walishindwa kukivuka.
Kufuatia ushindi huo Chelsea imeweka kibindoni kitita cha dola milioni 120 kinacholewa na Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA.