Chelsea, Fluminense zafuzu nusu fainali ya kombe la vilabu
5 Julai 2025Akizungumza kabla ya mechi ya hiyo leo Jumamosi, Kompany amesema PSG ya Luis Enrique na Bayern, mabingwa wa ligi za Ufaransa na Ujerumani mtawalia, hupendelea kumiliki mpira, kushambulia kwa nguvu na kuhimiza shinikizo la juu dhidi ya wapinzani wao.
Katika mechi nyengine Real Madrid inatarajia kushuka dimbani dhidi ya Borussia Dortmund. Kocha Niko Kovac amesema kikosi chake kimejiandaa vilivyo kupambana na Madrid.
Real Madrid haijawahi kufungwa na Borussia Dortmund katika mechi zao sita za mwisho walizokutana, wakishinda michezo minne mfululizo — ukiwemo ushindi wa 2-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka jana.
Mapema leo Chelsea imejikatia tiketi ya nusu fainali baada ya kuilaza Palmeiras ya Brazil mabao 2-1 na inasubiria kupambana na Fluminense iliyoifunga Al Hilal 2 - 1.