Changamoto za kuwania tiketi za kombe lijalo la Dunia Ujerumani
18 Agosti 2005Mapambano ya kirafiki kati ya Holland na Ujerumani, Brazil na Croatia, Uingereza na Denmark na Ufaransa na Ivory Coast.
Stadi wa Ghana Michael Essien mwishoe anajiunga na Chelsea ya uingereza kutoka Olympique Lyon kwa kitita cha hadi dala milioni 47 - rekodi kwa mchezaji wa Afrika.
Mganda Dorcus Inzukuru alieipatia Uganda medali yake ya kwanza ya dhahabu tnagu marehemu John Akiibua mjini Munich atunzwa na Bunge nishani ya shujaa wa Uganda - tunazungumza na waziri wa michezo wa Uganda juu ya tokeo hilo na jinsi wanachi walivyoushangiria wiki hii ushindi wake ndio madaa kuu wiki hii:
BUNDESLIGA - Ligi ya ujerumani imekaa kando mwishoni mwa wiki hii kutoa nafasi kwa duru ya kwsanza ya kombe la taifa la Ujerumani ambalo kama kombe la Ligi limo mikononi mwa mabingwa Bayern Munich.
Iliposita mwishoni mwa juma lililopita, Bayern Munich ikiongoza orodha ya Ligi hii ingawa kwa magoli tu-ikifuatwa nyuma na Bremen,S chalke na FC Cologne, miongoni mwa timu chipukizi zilizopanda daraja ya kwanza msimu huu ndio iliosisimua kwani imeanza vyema kabisa kuliko wenzake.Imeshinda kwanza bao 1:0 nyumbani dhidi ya Mainz na jumapili iliopita ikaizaba Stuttgart mabao 3-2 mjini Stuttgart.
Kati ya wiki hapo jumatano ikawa zamu ya kinyan’ganyiro cha kufuzu kwa kombe lijalo la dunia: Baadhi ya timu kama Ujerumani zilcheza mapambano ya kirafiki kwa shabaha lakini ilei le ya kujiwinda kwa kombe hilo la dunia.
Ujerumani iliingia uwanjani na mahasimu wao wa jadi Holland-timu mbili ambazo zilicheza finali 2 miaka ya nyuma:Ujerumani na Holland zilikumbana katika finali ya Kombe la dunia 1974 mjini Munich na Ujerumani ikashinda kwa mabao 2:1.
Ujerumani na Holland zikakutana tena katika finali ya kombe la Ulaya 1988 mjini Munich n amara hii Holland ikiwa na mshabulizi Marco van bastian,kocha wa leo wa holland ilishinda kwa mabao 2:0.
Jumatano basi Holland na Ujerumani zilikuwa na miadi nyengine mara hii mjini Rotterdam,nyumbani mwa wadachi. Wadachi walitangulia kutia mabao 2 kabla Ujerumani kusawazisha.
Mwishoe timu hizi mbili ziliondoka suluhu mabao 2:2. Holland inaongoza kundi lake linaloania tiketi ya kuja Ujerumani mwakani kwa kombe la dunia kwa pointi 1 ikifuatwa na Jamhuri ya Czech.
Ujerumani kama mwenyeji wa kombe hili inaingia finali mwakani bila kupingwa.
Mabingwa wa dunia Brazil lakini wanapaswa kukata tiketi yao kutoka kanda ya Amerika kusini na huko wako nyuma ya Argentina. Lakini hakuna shaka Brazil itakata tiketi yake ya kuja ujerumani kwani hadi sasa Brazil haikukosa kucheza katika kombe la dunia tangu lilipoasisiwa mjini Montevideo, Uruguay,1930.
Katika changamoto yao ya kujipima nguvu kati ya wiki hii, Brazil ilitoka sare bao 1:1 na Croatia. Ronaldo jogoo lao lilikosa mabao kadhaa wazi.
Mabingwa wengine wa dunia - Ufaransa wakiania bado tiketi yao ya Kombe la dunia, walipimana nguvu na Ivory Coast. Tembo hao wa africa huenda mara hii wakawanyima simba wa nyika – kamerun na kuja wao katika Kombe la dunia.Ufaransa lakini ikicheza na Zinedine Zidane alierejea kuvaa jazi ya timu ya taifa kama vile Claude Makelele na Lilion Thuram, iliwaponda tembo wa ivory Coast kwa mabao 3:0 bila majibu.
Didier Dragoba wa Chelsea alinawiri lakini kwa bahati mbaya hakutia bao. Kenya Harambee Stars ilizabwa bao 1:0 na mabingwa wa Afrika Tunesia mjini Tunis.Matumaini ya Harambee Stars kuja Ujerumani kwa Kombe lijalo la dunia yamepata mkosi mwengine. Tunesia inaelekea kupanga miadi ya mwisho na Morocco kuania tiketi ya Kombe la dunia. Sudan ilikuwa nyumbani na mcheza kwao hutunzwa: iliichapa Benin bao 1:0.
Mashaka yaliwakumba waingereza walipokutana na wadenimark kwa dimba la kirafiki: Uingereza ilizabw amabao 4:1. Kombe la dunia itatimilia. Uingereza ina miadi na Wales mjini Cardiff hapo septemba 3-mpambano wao wa Kombe la dunia unaofuatia pigo hilo kali kabisa isiowahi kupata uingereza tangu kupita miaka 25. Itakua sasa jukumu la kocha Eriksson sasa litakua kuepusha msukosuko mwengine england itakapoingia uwanjani na Wales.
Mshambulizi wa Ghana Michael Essien mwishoe amekata kiu chake wiki hii cha kucheza katika Premier League - ligi ya Uingereza. Kwani klabu yake ya Ufaransa Olympique Lyon iliregeza kamba na kumuachia kujiunga na Chelsea - mabingwa wa Uingereza. Lakini haikuwa kabla Chelsea kuridhia kulipa kitita kikubwa cha hadi dala milioni 47 kumkomboa chipukizi huyo wa miaka 22 kutoka Ghana. Iwapo nyota hii nyeusi – Black star- itanawiri kweli katika mawingu ya Ligi ya Uingereza kama ilivyonawirikatika ligi ya Ufaransa,yafaa kusubiri na kuona.
Pale Ghana ilipocheza kati ya wiki hii na Senegal, na kutoka suluhu 0:0, Essien alikuwa uwanjani lakini bila kucheza.
Stadi mwengine wa Afrika aligonga vichwa vya labari wiki hii: Mshambulizi Frederic Kanoute kutoka Mali alifunga mkataba wa dala milioni 8 kuihama Tottenham Hotspur na kujiunga na Se villa ya Spain.Stadi huyu mwenye umri wa miaka 27 amefunga mkataba wa miaka 4. Kanoute alianza maisha yake ya dimba na Olympique Lyon na akaichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya chipukizi kabla kuhamia kuichezea Mali katika Kombe la Africa la Mataifa lililopita.
Nae stadi wa zamani wa bafana Bafana Mark Fish alitangaza wiki hii anastaafu akliwa na umri wa miaka 31.Hii inafuatia kuumia kitambo kirefu goti.Mark Fish akiichezea Charlton Athletic nchini Uingereza.
Wakati wake katika Ligi ya Uingereza, Mark Fish alicheza mechi 204 baada ya kujiunga na Bolton Wandereres kutoka Lazio Roma ya Itali hapo 1997. Kabla ya hapo Mark Fish akiichezea Orlando Pirates ya Afrika Kuisini.
Tukimalizia na riadha:Uganda imejipatia malikia wa mbio za masafa ya mita 3000 kuruka viunzi: Dorcus Inzikuru ghafula amewastua waganda usingizini kwamba, kuna mastadi nchini kama marehemu John Akii-bua, alieshinda medali ya dhahabu na wakati huo huo kweka rekodi yxa olimpik katika michezo ya 1972 mjini Munich.
Miaka 33 baada ya Akki-bua, Dorcus Inzikuru amerudi Kampala na medali nyengine ya dhahabu kutoka Helsinkikatika masafa ya mita 3000 kuruka viunzi wanawake.