Morocco na nchi zingine 3 zatinga nusu fainali CHAN
24 Agosti 2025Matangazo
Katika mtanange wa nusu fainali za CHAN, Sudan itavaana na Madagascar jijini Dar es Salaam huku Morocco ikimenyana na mabingwa watetezi Senegal mjini Kampala. Mechi hizo zitachezwa Jumanne ya Agosti 26.
Mashabiki wa Afrika Mashariki wamehuzunishwa na kitendo cha mataifa yao wenyeji wa michuano hiyo ya CHAN ambayo ni Tanzania, Kenya na Uganda kushindwa kusonga mbele.