CHAN 2024: Harambee Stars yaishangaza Moroko
10 Agosti 2025Matangazo
Licha ya Moroko kutawala mwanzoni, Kenya walianza kuingia kwenye mchezo kupitia mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa Bryne Odhiambo na Ben Omondi. Hatimaye ari ya kujituma ilizaa matunda kunako dakika ya 41 wakati Ryan Wesley Ogam alipopachika wavuni bao la pakee na la ushindi katika mechi hiyo ya kundi A.
Harambee Stars wamepata ushindi huu wakiwa na wachezaji kumi baada ya Chrispine Erambo kuonyeshwa kadi nyekundu. Ushindi huu unaiweka Kenya katika nafasi ya kwanza kwenye jedwali la kundi A wakiwa na pointi saba.