SPD yaunga mkono kushirikiana kuunda serikali na CDU/CSU
9 Machi 2025Chama hicho hicho cha Social Democratic cha Ujeruman kimeutangaza uamuzi huo Jumapili mchana baada ya kufanya mkutano kwa njia ya mtandao.
Soma zaidi: Vyama vya CDU/CSU na SPD vyaanza mazungumzo ya awali ya kuunda serikali
SPD kimethibitisha kuwa muundo wa serikali ya pamoja kati yake na vyama hivyo utategemea matokeo ya kura ya wanachama itakayopigwa baadaye. Pande hizo mbili zilifanya mazungumzo ya awali Jumamosi ingawa SPD ilikosoa matokeo ya majadiliano hayo hasa kuhusu mipango ya kuongeza makali katika sera za uhamiaji na kuwabana zaidi waomba hifadhi.
Licha ya hilo vyama hivyo vimekubaliana katika masuala muhimu ya kifedha ikiwa ni pamoja na kufuta ukomo wa serikali kukopa katika matumizi ya ulinzi na mfuko maalumu wa uwekezaji na miundombinu wa euro bilioni 500.