SPD yaidhinisha makubaliano na muungano wa CDU/CSU
30 Aprili 2025Matangazo
Vyanzo vya ndani vya chama hicho zimesema asilimia 84.6 ya wanachama waliunga mkono makubaliano hayo katika kura iliyofanyika kwa kipindi cha wiki mbili na kuhitimishwa Jumanne.
Soma pia: Merz akaribia kushika usukani wa kuiongoza Ujerumani
Chama cha SPD kinatarajiwa kuwa mshirika mdogo katika serikali ijayo pamoja na muungano wa kihafidhina wa vyama vya Christian Democratic Union, CDU na Christian Social Union CSU, ambao pia tayari umeidhinisha makubaliano ya muungano huo.
Merz anatarajiwa kuchaguliwa kuwa Kansela mnamo Mei 6 katika kikao cha bunge la Ujerumani, Bundestag, takriban miezi miwili baada ya muungano wa CDU/CSU kushinda uchaguzi mkuu wa mwezi Februari.