Chama cha Le Pen chaitisha maandamano Ufaransa
1 Aprili 2025Matangazo
Mkuu wa chama cha mrengo mkali wa kulia nchini Ufaransa cha National Rally Jordan Bardella, amewatolea wito Wafaransa waandamane mwishoni mwa juma hili kupinga hukumu ya kumpiga marufuku Marine Le Pen asigombee nafasi ya afisi ya umma kwa miaka mitano baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa fedha za Umoja wa Ulaya.
Bardella alitoa taarifa chache kuhusu maandamano hayo mbali na kusema watagawa vipeperushi na kufanyika mikutano kila mahali nchini Ufaransa.
Hukumu ya jana Jumatatu ni pigo kwa Le Pen, kiongozi wa muda mrefu wa chama cha National Rally, ambaye amekuwa mbele katika kura za maoni kuelekea uchaguzi wa rais 2027.