Chama cha Labour chashinda uchaguzi Norway
9 Septemba 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa chama cha Labour nchini NorwayJonas Gahr Store ametangaza ushindi kufuatia uchaguzi wa bunge uliofanyika jana Jumatatu.
Waziri Mkuu huyo amesema wamefanikiwa kupata ushindi baada ya chama cha Labour kuwa cha kwanza na kiasi asilimia 28 ya kura ambazo zilimuwezesha abaki madarakani kwa kusaidiwa na vyama vingine vinne vya siasa za mrengo wa kushoto.
Store ataiongoza nchi hiyo ya eneo la Scandinavia kwa miaka mingine minne.
Uchaguzi wa Norway ulishuhudia ongezeko kubwa la uungaji mkono wa chama cha kizalendo cha Progess kinachopinga uhamiaji. Kufuatia matokeo ya uchaguzi chama hicho kimekuwa cha pili kwa ukubwa bungeni hali inayoibua wasiwasi.