Chama cha Kijani Ujerumani chakamilisha ilani ya uchaguzi
27 Januari 2025Katika mkutano wake jana Jumapili, chama hicho kilikubaliana kuhusu masuala mbalimbali, kuanzia uchumi hadi gharama za ulinzi na hata ufyatuaji wa fataki. Mpango wa chama cha Kijani unatoa wito wa kurahisisha kile kinachojulikana kama "ukomo wa deni," ambao unaweka vikwazo vikali kwa kiasi ambacho serikali inaweza kukopa na umelaumiwa kwa kuubinya uwekezaji wa umma.
Pia wanataka kuunda kile kinachojulikana kama mfuko wa Ujerumani ambao utawezesha uwekezaji wa muda mrefu katika barabara na madaraja, miundo mbinu ya reli na usafiri wa umma. Kikubwa zaidi asilimia 2%" ya pato la ndani inapaswa kuwekezwa katika uwezo wa usalama na ulinzi.
Kuhusu uhamiaji, Wanamazingira hao wanakubali kwamba Ujerumani ni nchi ya uhamiaji, lakini wakati huo huo wanasisitiza kwamba wale ambao hawana haki ya kukaa lazima waondoke.