SiasaChad
Chama cha Mahamat Idriss Deby chashinda uchaguzi, Chad
5 Machi 2025Matangazo
Hayo ni kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotolewa hapo jana.
Uchaguzi huo ulikuwa hatua ya mwisho ya mageuzi ya kisiasa yenye lengo la kujiimarisha zaidi, mageuzi ambayo yalianza wakati Deby alipochukua mamlaka baada ya kifo cha baba yake miaka minne iliyopita.
Deby alishinda muhula wa miaka mitano kama rais mwezi Mei mwaka jana katika uchaguzi uliosusiwa na upinzani huku mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yakiutaja kutokuwa huru wala wa kuaminika.