Chama cha AfD chafungua kesi kupinga uamuzi wa BfV
5 Mei 2025Matangazo
Mahakama ya Ujerumani imesema leo kwamba chama cha siasa kali za mrengo wa kulia,cha AfD kimefungua kesi ya kupinga uamuzi uliotangazwa na shirika la ujasusi wa ndani la Ujerumani,uliokiweka chama hicho katika orodha ya makundi ya itikadi kali.
Mahakama ya mjini Kolon imesema kesi pamoja na malalamiko ya AfD yatapitiwa mara shirika hilo la Ujasusi wa ndani nchini,BfV litakapothibitisha kupokea taarifa.
Hatua ya kuorodheshwa kwenye makundi ya itikadi, chama hicho kikuu cha upinzani bungeni, ilitangazwa Ijumaa iliyopita na inatowa nafasi kwa shirika hilo kuimarisha juhudi za kukifuatilia.
Bunge la Ujerumani pia huenda sasa likajaribu kuzuia ufadhili wa chama hicho.