Chad yaidhinisha katiba mpya baada ya kura ya maoni
29 Desemba 2023Mahakama ya juu ya Chad imetangaza matokeo ya kura ya maoni ya Desemba 17 siku ya Alhamisi ambayo ilipitishwa kwa asilimia 85.9 za kura dhidi ya kura asilimia 14.1 zilizoipinga. Idadi ya wapiga kura waliojitokeza ilikuwa asilimia 63.75.
Upinzani uliwasilisha ombi la kupinga matokeo
Kulingana na mahakama hiyo ya juu, upinzani uliwasilisha ombi la kupinga matokeo yakura hiyo na kuvunjiliwa mbali kwa tume ya maandalizi ambayo umeituhumu kwa kuwa na upendeleo.
Hata hivyo mahakama hiyo imekataa ombi hilo.
Soma pia:Chad yafanya kura ya maoni kuamua kuhusu katiba mpya
Kwa kutangazwa kwa matokeo hayo ya mwisho ya kura hiyo ya maoni, katiba hiyo mpya lazima sasa itangazwe na Rais wa mpito Mahamat Idriss Déby Itno ndani ya masaa machache.
Rais Déby ameahidi uchaguzi kufanyika mwaka ujao.