CDU/CSU waapa kuupigia kura muswada tata wa uhamiaji
31 Januari 2025Matangazo
Kiongozi wake, Friedrich Merz, amewaambia wabunge wa chama chake kwenye mkutano wa ndani, hii ikiwa ni kulingana na vyanzo mbalimbali vilivyozungumza na shirika la habari la DPA kwamba ni lazima wafanye maamuzi hii leo.
Soma pia:Angela Merkel akikosoa chama chake kwa kushirikiana na AfD kupitisha hoja bungeni
Matamshi hayo ya Merz anayetarajiwa kuwa kansela katika uchaguzi wa Februari 23, yalipokelewa kwa bashasha, vimesema vyanzo vya habari.
Merz ameapa kuweka sheria kali dhidi ya uhamiaji kwenye kura hiyo iliyoibua ghadhabu nchini Ujerumani kwa kuwa huenda akahitaji uungwaji mkono wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD.