CDU/CSU na SPD kuanza mashauriano ya kuunda serikali
13 Machi 2025Matangazo
Makundi 16 yenye wajumbe 16 kutoka vyama vyote hivyo wataanza leo mashauriano kuhusu mipango ya kina ya serikali ya mseto itakayoundwa.
Makundi hayo yatakutana kwa siku 10 na mapendekezo yao yatawasilishwa mbele ya timu maalum ya majadiliano itakayowajumuisha viongozi wakuu wa kila chama, kabla ya hatimae muswaada wa makubaliano yaliyofikiwa kuidhinishwa na vyama hivyo vitatu.
Soma pia:Mazungumzo ya kuunda serikali ya pamoja kati ya CDU/CSU na SPD yaanza Ujerumani
Chama cha SPD kimeshasema kwamba kitahitaji pia kushauriana na wanachama wake kuhusu makubaliano yatakayofikiwa,wakati Fredrich Merz kiongozi wa CDU akisema azma yake ni kuunda serikali mpya kufikia Pasaka.