CARACAS: Iran yapuza vichecheo vya kiuchumi
13 Machi 2005Matangazo
Iran inadhamiria kuendelea na mradi wake wa kinuklia licha ya Marekani kuimotisha kiuchumi ili iachilie mbali mpango huo unaoweza baadae kutumiwa kutengeneza silaha za atomu.Rais Mohammad Khatami wa Iran akizungumza Caracas,mji mkuu wa Venezuela amesema nchi yake haitoachilia mbali haki zake.Lakini Tehran ipo tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuondosha khofu kuwa Iran inatengeneza silaha za kinuklia.Marekani ikiziunga juhudi za kidplomasia za Ulaya ilitangaza vichecheo vya kiuchumi kwa Iran pindi itasitisha mpango wake wa kinuklia.Uingereza,Ujerumani na Ufaransa zinaongoza majadiliano pamoja na Iran inayoshinikizwa kuwa isitishe kuzalisha uranium inayoweza pia kutumiwa kutengeneza silaha za kinuklia.