Canada yaahidi kushinda vita vya kibiashara dhidi ya US
10 Machi 2025Carney ameyasema hayo mara tu baada ya kutangazwa mshindi kwa asilimia asilimia 85.9 ya kura zilizopigwa kwenye uchaguzi wa uongozi wa Chama cha kiliberali ambacho kinaitawala nchi hiyo.
"Wamarekani wanataka rasilimali zetu, maji yetu, ardhi yetu na hata nchi yetu. Na kama wangefaulu, wangeharibu mfumo wetu wa maisha. Huko Marekani,huduma za afya ni biashara kubwa lakini hapa kwetu hiyo ni haki ya msingi kwa kila mtu. Marekani sio Canada na haitawezekana kwa namna yoyote ile Canada kuwa sehemu ya Marekani."
Soma pia:Mark Carney kuwa Waziri Mkuu mpya nchini Canada
Mark Carney ambaye ni gavana wa zamani wa Benki Kuu nchini humo anamrithi Justin Trudeau, aliyetangaza kujiuzulu mwezi Januari baada ya kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka tisa. Katika hotuba yake ya kuaga Justin Trudeau amesema Wacanada wanakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa nchi jirani ambayo ni Marekani.