Canada kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za Marekani
2 Februari 2025Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema hii leo kwamba nchi yake itaanzisha ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazotoka nchini Marekani kama njia ya kulipiza kisasi kufuatia hatua ya Marekani ya kuweka ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka nchini mwake.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Trudeau amesema hatua hiyo ya Marekani inazitenganisha zaidi nchi hizo mbili badala ya kuzifanya kuwa karibu.
Amesema iwapo Marekani inataka kufanikisha enzi mpya ya ustawi inapaswa kushirikiana zaidi na Canada na siyo kuwaadhibu kwa ushuru.
Soma zaidi. Trump atishia kuziwekea nchi za BRICS ushuru wa asilimia 100
Siku ya Jumamosi, Rais wa Marekani Donald Trump alisaini agizo la kuanzisha ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za Mexico na Canada huku asilimia 10 ikiwa ni kwa bidhaa za China.
Kwa upande mwingine ikulu ya White House imesema ushuru huo ni majibu kwa nchi hizo tatu ambazo zinaruhusu dawa haramu kuingia nchini Marekani