Cambodian na Thailand zakubaliana kusitisha mapigano
28 Julai 2025Waziri mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim ambaye aliongoza mazungumzo hayo kama mkuu wa Muungano wa kikanda wa Mataifa ya kusini- mashariki mwa Asia , amesema pande zote mbili zimefikia muafaka wa kuchukua hatua za kurejea katika hali ya kawaida kufuatia kile alichokitaja kuwa majadiliano ya kweli.
Viongozi wa Thailand, Cambodia kukutana Malaysia
Akisoma taarifa ya pamoja ya waziri mkuu wa Cambodia Hun Manet na kaimu waziri mkuu wa Thailand Phumtham Wechayachai, Anwar amesema wamekubaliana kusitisha mapigano hayo kuanzia saa sita usiku ya Jumanne kwa majira ya eneo hilo.
Mzozo wa mpakani Thailand na Cambodia wazidi makali
Pia amesema maafisa wa kijeshi kutoka pande zote pia watafanya mikutano ya kutuliza mvutano katika maeneo ya mipaka.
Hun Manet na Phumtam wamepongeza matokeo ya mkutano huo na kusalimiana kwa mikono wakati wa kuhitimisha mkutano mfupi na waandishi wa habari.