CAIRO: Waziri wa nje wa Ujerumani Joshka Fischer,...
16 Desemba 2003Matangazo
amewataka waisrael na wapalestina kurejea katika m eza ya mazungumzo. Akizungumza na maripota baada ya mkutano wake na rais Hosni Mubarak mjini Cairo leo, Fischer amesema kurejea kwenye meza ya mazungumzo ndio njia pekee iliopo.Akasema Misri ina mchango mkubwa wa kutoa.Baadae hii leo, waziri huyo wa nje wa Ujerumani akitarajiwa kuonana na waziri wa nje wa Jordan Marwan Moasher mjini Amman. Kesho,Fischer atafunga safari hadi jeruselem kwa mazungumzo na waziri m kuu wa Israel, Ariel Sharon kabla mkutano na waziri m kuu wa palestina Ahmed Qorei.