CAIRO : Maandamano yageuka vurugu
31 Julai 2005Matangazo
Maandamano ya upinzani mjini Cairo juu ya Rais Hosni Mubarak yamegeuka kuwa ya vurugu wakati polisi wa kutuliza ghasia na wafuasi wa serikali walipowashambulia waandamanaji hapo jana.
Makundi ya upinzani nchini Misri yameitisha maandamano hayo dhidi ya kuteuliwa kwa Mubarak kugombania Urais kwa kipindi cha sita.Kuteuliwa huko kumekuja siku moja baada Rais kutangaza kwamba atagombania kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa kwanza wa Rais wa vyama vingi hapo mwezi wa Septemba.
Kwa mujibu wa mashahidi askari kanzu waliwapa mkon’goto waandamanaji na kuwaburuza kwenye magari.
Zaidi ya watu 30 wametiwa mbaroni.