BUSH-UHUSIANO MAALUM NA UINGEREZA:
22 Novemba 2003Matangazo
WASHINGTON: Rais George W.Bush wa Marekani amerejea nyumbani baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Uingereza.Amesema ziara hiyo ilitoa fursa kwa Marekani na Uingereza kuzungumza juu ya njia za kupigana dhidi ya ugaidi.Akaongezea kuwa kati ya nchi yake na Uingereza kuna,kile alichokiita kuwa ni uhusiano maalum.Siku ya Alkhamis mjini London watu laki moja waliandamana kulalamika dhidi ya msimamo wa rais Bush na waziri mkuu Tony Blair wa Uingereza kuhusu suala la Iraq.